MOSCOW: Urusi yasema haiko tayari kujadili hatima ya Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 03.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Urusi yasema haiko tayari kujadili hatima ya Kosovo

Urusi imeashiria kwamba haiko tayari kujadiliana kuhusu hatima ya jimbo la Kosovo na mpango wa Marekani kutaka kujenga mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora barani Ulaya.

Akiwahutubia wanafunzi katika taasisi ya maswala ya kimataifa mjini Moscow, waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, ameieleza hatima ya Kosovo na mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora mashariki mwa Ulaya kuwa maswala tete ambayo hayapaswi kujadiliwa.

Urusi inapinga mpango unaoungwa mkono na nchi za magharibi unaotaka jimbo la Kosovo liwe huru kutoka kwa Serbia ikisema itakubali tu suluhisho kuhusu hali ya baadaye ya jimbo hilo litakaloungwa mkono na serikali ya mjini Belgrade na Waalbania wa Kosovo walio wengi.

Urusi pia inasema mpango wa Marekani kujenga mifumo ya ulinzi dhidi ya Iran na Korea Kaskazini barani Ulaya ni tishio kwake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com