1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Urusi yafukuza wanadiplomasia 4 wa Uingereza

19 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBh0

Urusi imearifu kuwa inawafukuza wanadiplomasia 4 wa Kingereza,kujibu hatua iliyochukuliwa na Uingereza kuwafukuza wanadiplomasia 4 wa Kirusi. Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya masuala ya nje wa Urusi,Mikhail Kamynin,mbali na hatua hiyo, Urusi itazuia kutoa vibali vya kusafiri kwa maafisa wa Kingereza na vile vile itasitisha ushirikiano wake na Uingereza kupambana na ugaidi.

Mgogoro huo unahusika na mauaji ya mwaka jana ya wakala wa zamani wa Kirusi,Alexanader Litvinenko ambae alikuwa mkosoaji wa serikali ya Moscow. Waendesha mashtaka wa Kingereza wanamshuku wakala wa zamani wa Kirusi,Andrei Lugovoi kuhusika na mauaji hayo na waliitaka Moscow imwasalishe Uingereza;ombi lililokataliwa na Urusi.Moscow inasisitiza kuwa katiba ya nchi hairuhusu kuwapeleka raia wake katika nchi nyingine. Litvinenko,kabla ya kufariki aliilaumu serikali ya Urusi na kusema kuwa ndio iliyotoa amri ya kumuua.