MOSCOW: Ripota wa Kirussi ameuawa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Ripota wa Kirussi ameuawa

Polisi nchini Urussi wamechukua kompyuta na nyaraka za muandishi wa habari Anna Politkovskaya,alieuawa Moscow,siku ya Jumamosi kwa kupigwa risasi.Kwa mujibu wa wafanyakazi wenzake,Politkovskaya alikuwa akitayarisha ripoti juu ya vitendo vya mateso katika jimbo la Chechnya.Makamu wa mhariri mkuu wa gazeti la “Novaya Gazeta” mjini Moscow amesema,ripoti hiyo ilitazamiwa kuchapishwa siku ya Jumatatu. Politkovskaya,alikutikana amepigwa risasi ndani ya lifti ya jengo alikoishi mjini Moscow.Polisi wamekuta bastola na risasi kando ya mwandishi wa habari huyo aliekuwa maarufu kwa uchunguzi wake na ukosoaji wa serikali ya Moscow na vita vya Chechnya.Baraza la Umoja wa Ulaya limelaani shambulio hilo na limetoa wito wa kuchunguza tukio hilo kwa haraka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com