1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Putin kumtaja mrithi wake mwezi ujao

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, anatarajiwa kumtaja mrithi wake mwezi ujao. Hayo ni kwa mujibu wa Sergei Ivanov, naibu wa kwanza wa waziri mkuu wa Urusi.

Srgei Ivanov ameuambia ujumbe wa wasomi wa Urusi katika nchi za kigeni kwamba chama tawala kitatangaza mgombea wake wa wadhifa wa urais katika uchaguzi wa mwaka ujao wakati kitakapofanya mkutano wake wa kila mwaka mwezi ujao.

Tangazo hilo limetolewa baada rais Putin kumteua mtalamu wa fedha, Viktor Subkov, kushika wadhifa wa waziri mkuu baada ya kuivunja serikali ya waziri mkuu, Mikhail Fradkov. Rais Putin amesema

´Urusi inakaribia uchaguzi wa bunge utakaofuatiwa na uchaguzi wa rais. Ipo haja ya kufikiria vipi tunavoweza kufanya mabadiliko katika serikali ili kujiandaa kwa kipindi cha uchaguzi na vipi nchi inavyotakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa bunge na wa rais mwezi Machi mwaka ujao.´

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com