1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Polisi waweka doria kuzuwia maandamano.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCw4

Maafisa nchini Russia wameweka polisi kadha mjini Moscow kuzuwia watu wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia kujikusanya kwa ajili ya siku iliyotangazwa nchini humo ya umoja wa kitaifa.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa polisi wamewakamata watu kadha karibu na kituo kikuu cha treni cha Kultury, ambako watu hao wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia walipanga kufanya maandamano dhidi ya wahamiaji ambao sio wenye asili ya Russia licha ya kupigwa marufuku kwa maandamano hayo.

Wakati huo huo , kiasi cha watu 200 wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia wamefanya maandamano kupitia mitaa mikuu ya mji wa Novosibirsk katika jimbo la Siberia, wakitoa kauli mbiu na kupepea bendera zilizo za alama ya mafashist mamboleo. Watu kumi waliotayarisha maandamano hayo wamekamatwa.