Moscow. Mwandishi wa habari maarufu akutwa ameuwawa.
8 Oktoba 2006Matangazo
Mwandishi wa habari za kiuchunguzi ambaye anafahamika kwa taarifa zake za ukosoaji wa serikali ya Russia katika vita na jimbo linalotaka kujitenga la Chechnya amekutwa amepigwa risasi na kufa mjini Moscow.
Polisi wanasema mwili wa Anna Politkovskaya uligunduliwa katika ngazi za jengo anamoishi, pamoja na silaha iliyomuua na risasi nne zilizokwisha tumika.
Amefariki kutokana na kupigwa risasi kadha kwa masafa ya karibu.
Baraza la ulaya limetaka kufanyike haraka uchunguzi kamili wa mauaji hayo.