1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Mwanaharakati wa upinzani akamatwa

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9z

Mwanaharakati wa upinzani nchini Urusi amekamatwa baada ya kuhudhuria maandamano.

Garry Kasparov bingwa wa zamani katika mchezo wa Chess alisimamishwa pamoja na wafuasi wengine walipojaribu kulifikia eneo jekundu ambapo kulikuwa na maelfu ya waandamanaji wanaopinga utawala wa Kremlin.

Takriban polisi alfu 9 wa kupambana na ghasia wamepelekwa katika sehemu mbalimbali za mji mkuu wa Mosko kudhibiti ghasia.