1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Abbas ziarani Urusi

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdn

Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, anafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Urusi. Hii leo atakutana na waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Moscow.

Rais Abbas pia anatarajiwa kukutana na rais wa Urusi, Vladamir Putin, wakati wa ziara yake kuzungumzia matatizo yanayoendelea katika maeneo ya Wapalestina.

Abbas aliwasili jana mjini Moscow katika zaira ya kwanza tangu kundi la Hamas lilipolidhibiti eneo la Ukanda wa Gaza mnamo mwezi Juni mwaka huu na anatazamia kumshawishi rais Putin amuunge mkono pamoja na chama chake cha Fatah.

Rais Abbas amesema urafiki baina ya Urusi na Palestina ni wa kihistoria na Wapalestina wataendelea kuulinda na kuuimarisha.

Urusi ni mwanamchama wa pande nne zinazoudhamini mpango wa amani ya Mashariki ya Kati zikiwemo pia Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.