1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MORONI:Uchaguzi wa rais waahirishwa Anjouan

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBti

Uchaguzi wa rais umeahirishwa kwa wiki moja katika kisiwa cha Nzouani huko Komoro.Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika jumapili hii na kuahirishwa kufuatia ghasia za kisiasa pale polisi walipowapiga risasi raia wawili.

Komoro ilipanga kufanya uchaguzi wa rais wa kila kisiwa Ngazija,Moheli na Nzouani.Kwa mujibu wa serikali kuu uchaguzi wa rais katika visiwa vya Moheli na Ngazija unaendelea kama ilivyopangwa mwishoni mwa juma hili ila wa Nzouani unafanyika tarehe 17 mwezi huu.

Visiwa vyote vitatu vitafanya awamu ya pili ya uchaguzi tarehe 24 mwezi huu.Watu watatu walijeruhiwa siku ya Jumanne wakati polisi kisiwani Nzouani walipofyatua risasi katika umati uliosubiri kulaki ndege ya rais wa Shirikisho wa Komoro Ahmed Abdullah Mohammed Sambi.Rais Sambi alilazimika kurudi wakati ndege yake iliposhindwa kutua.

Vuta ni kuvute imeendelea kisiwani humo tangu majeshi ya kiongozi wa zamani Mohamed Bacar kusababisha vifo vya wanajeshi wawili wa shirikisho mwezi Mei.

Visiwa hivyo vitatu vilivyo na idadi ya watu laki sita na sabini vina uhuru wa kujingoza na kuwa na rais na bunge kwa kila kisiwa kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2001.Kulingana na makubaliano hayo rais wa shirikisho anateuliwa na kila kisiwa kwa kupokezana.