MORONI : Bakar kuwania Urais wa Anjouan | Habari za Ulimwengu | DW | 13.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MORONI : Bakar kuwania Urais wa Anjouan

Kiongozi wa uasi wa zamani wa kisiwa cha pili kwa ukubwa cha Comoro atawania tena madaraka katika uchaguzi wa mwezi ujao baada ya kujiuzulu kumaliza uasi mdogo.

Mohamed Bakar rais wa kisiwa cha Anzuani mojawapo ya visiwa vitatu vya Comoro vyenye mamlaka fulani ya kujitawala amekubali hapo Ijumaa kutii amri ya mahkama ya katiba kwamba muda wake wa miaka mitano umemalizika.

Kugoma kuachia madaraka kwa Bakari hapo awali kulipelekea mapigano kati ya vikosi vyake na wanajeshi wa serikali kuu na kuzusha hofu kuelekea uchaguzi wa arais wa visiwa hivyo.

Visiwa vyote vitatu kisiwa kikuu cha Ngazija,Anzuani na Moheli ambavyo idadi yake ya watu ni kama 670,000 vinapiga kura tarehe 10 Juni na tarehe 24 Juni iwapo kutahitajika duru ya pili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com