1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monchengladbach yaikaribisha Schalke

26 Agosti 2011

Monchengladbach inawania kuendeleza mwanzo wake mzuri msimu huu, wakati inajitayarisha kuikaribisha Schalke 04

https://p.dw.com/p/12OQA
Filip Daemswa MonchengladbachPicha: dapd

Timu ya Monchengladbach inaendelea kuishikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya ligi hiyo wakati inajitayarisha kuikaribisha Schalke 04 Jumapili.

FC Schalke 04 vs. HJK Helsinki
Shabiki wa SchalkePicha: picture-alliance/dpa

Timu hiyo iliyo chini ya ukufunzi wa Lucien Favre tangu mwezi February mwaka uliopita, ilikuwa chini kwenye orodha ya ligi hiyo na ilikuwa na udhaifu mkubwa katika kiungo cha ulinzi katika historia ya ligi hiyo.

Ilipoteza magoli 56 katika mechi 22.

Shukrani lukuki zinamuangukia kocha huyo wa kutoka Uswisi kwa mageuzi makubwa aliyo yafanya kwa kuanza kwa ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Schalke.

Fussball Bundesliga Saison 2011 2012 3. Spieltag Borussia Moenchengladbach - VfL Wolfsburg im Borussia Park
Marco Reus, kulia , na kipa Marc-Andre Ter Stegen wa MonchengladbachPicha: dapd

Schalke kwa upande wake ipo katika nafasi ya nne kwenye orodha hiyo ya Bundesliga, na inatazamia kuihangaisha Monchengladbach na kukipa kiungo cha ulinzi cha timu hiyo mtihani, baada ya ushindi wake wa mabao 5 dhidi ya Cologne na 4 dhidi ya Mainz wiki iliyopita.

Hannover 96 inaikaribisha Mainz.

Pambano linalotarajiwa Jumamosi jioni ni lile kati ya Bayer Leverkusen na timu bingwa mtetezi Borussia Dortmund.

Timu iliyokuwa mshindi wa pili msimu uliyopita, Bayer Leverkusen haijawahi kufungwa nyumbani katika ligi hiyo tangu ilipofungwa 3-1 na Dortmund mnamo mwezi Januari.

Mwandishi: Maryam, Abdalla/Afpe/Ape.
Mhariri:Josephat, Charo.