MOGADISHU:Uhuru wa waandishi wa habari wakandamizwa | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Uhuru wa waandishi wa habari wakandamizwa

Shirkisho la kimataifa la waandishi wa habari limeilaumu serikali ya mpito ya Somalia kwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Waziri wa habari wa Somalia Madobe Nurrow Mohamed ametoa amri kwamba vyombo vya habari vya nchini humo vijiorodheshe katika ofisi yake, vyombo vya habari vya kimataifa sasa havitaruhusiwa kufanya kazi na vyombo vya habari au waandishi wa Somalia kabla ya kupata ruhusa kutoka kwenye wizara ya habari.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yametoa mwito wa kulindwa waandishi wa habari nchini Somalia ambako takriban wandishi saba wameuwawa mwaka huu na waandishi wengine kadhaa wamekamatwa na kuwekwa kizuizini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com