MOGADISHU:Shemejiye waziri mkuu auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Shemejiye waziri mkuu auwawa

Nchini Somalia shemeji yake Waziri mkuu Ali Mohammed Gedi, Yusuf Mohammed Dhisow ameuwawa hapo jana katika mashambulio mabaya ya karibuni.

Hali hiyo inatokea wakati Umoja wa Afrika unataarisha wanajeshi wa kulinda amani nchini humo.

Washambuliaji hao waliimpiga risasi bwana Yusuf ambaye alikuwa akiendesha gari lake katika eneo la soko kuu ya Mogadishu ya Bakara,kusini mwa mji huo.

Kwa mujibu wa jamaa ya Yusuf, alilengwa kutokana na uhusiano wake na waziri mkuu Ali Gedi na kuna hofu kubwa kwamba maafisa wa serikali pamoja na jamaa zao wanalengwa na mashambulio nchini humo.

Somalia bado inasubiri wanajeshi wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani mjini Mogadishu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com