1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mfanyikazi wa WFP aachiwa Huru

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DI

Serikali ya Somalia imemuachia huru mfanyikazi wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula WFP baada ya kumtia kizuizini kwa muda wa wiki moja.

Wanajeshi kadhaa wa usalama walivamia afisi za shirika hilo mjini Mogadishu jumatano iliyopita na kumtia mbaroni Idriss Osman mkuu wa shughuli za kutoa msaada nchini humo bila ya kutoa sababu za kumkamata kwa WFP.

Hata hivyo maafisa wa serikali walisema walikuwa wakitaka kumchunguza Osman kwa kile kisichojulikana.

Kukamatwa kwa Osman kulizusha shutuma kali kutoka jumuiya ya kimataifa dhidi ya serikali ya mpito ya Somalia.