Mogadishu.Mapigano yazuka huko Puntland nchini Somalia. | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu.Mapigano yazuka huko Puntland nchini Somalia.

Mapigano yameripuka hii leo kati ya vikosi vya itikadi kali za kiislamu na vikosi vya jeshi, katika mkoa wa Kaskazini wa Puntland nchini Somalia unaopinga ushawishi wa wafuasi wa itikadi kali za kiislamu.

Wakizungumza na shirika la habari la Reuters wapiganaji wa Kiislamu wamesema kuwa wameshambuliwa na vikosi vya jeshi la Puntland muda mchache uliopita katika eneo la Galinsoor.

Hakukuwa na taarifa zaidi zilizoripotiwa za maafa licha ya kuzuka khofu ya kufufuka upya kwa mapigano baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya amani wiki iliyopita.

Viongozi wa Puntland wamesema kuwa, watazuia harakati zozote za wapiganaji wa Kiislamu za kutaka kujiimarisha katika mkoa wa Kaskazini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com