1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Al Qaida yateua kamanda huko Somalia

Serikali ya mpito ya Somalia imesema kuwa kundi la Al Qaida, limemteua kamanda kijana wa wapiganaji wa kiislam kuwa kiongozi wake katika nchi hiyo ya pembe ya afrika.

Waziri wa Ulinzi wa serikali hiyo Jalal Ali Jelle amesema kuwa, kijana huyo, Aden Hashi Ayro mwenye umri wa miaka 30 na mzaliwa wa Afghanistan ni komandoo aliyefuzu.

Amesema kuwa Aden ni kiongozi wa kundi linaloagopwa la Shabab na amekuwa akihusika na kuongezeka kwa mapigano.

Kauli hiyo ya waziri wa ulinzi wa Somalia inakuja mnamo wakati nchi hiyo imeingia katika siku ya pili ya mapigano makali mjini Mogadishu.

Marekani na Somalia kwa muda mrefu zimekuwa zikimlaumu Hashi Ayro na viongozi wengine wa mahakama za kiislam kuhusika na mtandao wa Al Qaida

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com