1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wanajeshi wa Uganda wameuawa Somalia

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1T

Nchini Somalia,wanajeshi 4 wa Uganda wa vikosi vya Umoja wa Afrika wameuawa katika mripuko wa bomu uliotokea kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu. Wengine 5 pia walijeruhiwa katika mripuko huo ulitokea kando ya barabara ambako mlolongo wa magari ya walinzi wa amani wa Uganda ulikuwa ukipita.Uganda imepeleka Somalia wanajeshi 1,500 kulinda amani,kama sehemu ya wanajeshi 8,000 ambao Umoja wa Afrika unahangaika kukusanya. Mashambulio dhidi ya vituo vya kiraia yameongezeka,tangu vikosi vya serikali ya Somalia na vya Ethiopia kuwatimua wanamgambo wa Kiislamu kutoka maeneo ya kati na kusini ya Somalia mwanzo wa mwaka huu.Kwa upande mwingine ripoti zinasema kuwa nje ya pwani ya Somalia,watu wenye bunduki wameteka nyara boti mbili za uvuvi za Korea ya Kusini.Kwa mujibu wa wizara ya nje ya Korea ya Kusini,kiasi ya watu 30 wamo katika boti hizo,4 ni raia wa Korea ya Kusini.