MOGADISHU: Walinzi wa amani wameuawa Somalia
16 Mei 2007Matangazo
Nchini Somalia,si chini ya wanajeshi 4 wa Uganda wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa baada ya vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika kushambuliwa katika mji mkuu Mogadishu.Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Afrika,bomu liliripuliwa kando ya barabara,ulipopita mlolongo wa magari ya vikosi vya amani.