MOGADISHU: Umwagaji wa damu waendelea Somalia
29 Machi 2007Matangazo
Si chini ya watu 11 wameuawa katika mapigano makali yaliyozuka mji mkuu wa Somalia,Mogadishu. Kwa mujibu wa ripoti za waandishi wa habari, helikopta na vifaru vya majeshi ya Ethiopia mapema leo asubuhi vilishambulia ngome ya waasi kusini mwa mji mkuu Mogadishu.Wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu waliotimuliwa na vikosi vya serikali ya Somalia na Ethiopia,wanalaumiwa kuhusika na machafuko ya umwagaji damu katika mji huo mkuu.