1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Uhuru wa vyombo vya habari wabanwa

20 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQd

Serikali ya Somalia imepiga marufuku vyombo vya habari visiripoti harakati za kijeshi na maswala ya wakimbizi.

Afisa wa usalama, Nour Mohammed Mahmoud, amesema serikali itawataja wahariri wake watakaofanya kazi katika vituo vitatu vya redio nchini humo. Serikali pia imeanzisha kikosi cha kupambana na ugaidi kukabiliana na ongezeko la machafuko mjini Mogadishu.

Naibu spika wa bunge la Somalia, Mohamed Omar Dalha, amesema vikosi vipya vitawajulisha polisi waliopokea mafunzo maalumu na wanajeshi watakaokuwa na magari ya mfano wa vifaru yatakayobeba silaha nzito za kisasa.

Mashambulio mapya ya makombora baina ya wanamgambo na vikosi vya serikali yalisabisha vifo vya watu wasiopungua watatu hapo jana.