MOGADISHU: Ugomvi wa kurithi wasababisha vifo 20 | Habari za Ulimwengu | DW | 19.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Ugomvi wa kurithi wasababisha vifo 20

Watu wasiopungua 20 wameuawa na darzeni kadhaa wamejeruhiwa baada ya ugomvi kuzuka kati ya makundi mawili yaliyokuwa yakigombea visima vya maji.Kwa mujibu wa mashahidi,ugomvi huo unahusika na uadui wa kurithi,baina ya makabila mawili na si uasi unaoongozwa na wanamgambo katika mji mkuu Mogadishu.

Katika tukio jingine,mashahidi wamesema,mwanamke mmoja aliuawa siku ya Jumamosi katika soko la Bakara mjini Mogadishu.Katika shambulizi hilo, polisi waliokuwa wakipiga doria walirushiwa gruneti na inashukiwa kuwa waasi ndio waliohusika na shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com