1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Rais Yusuf awasili Mogadishu

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcI

Rais wa serikali ya mpito ya Somalia, Abdulahi Yusuf Ahmed, amewasili mjini Mogadishu kwa mara kwanza tangu alipochaguliwa mnamo mwaka wa 2004. Rais Yusuf alikaribishwa na waziri mkuu, Ali Mohammed Gedi, katika uwanja wa ndege wa mjini Mogadishu.

Ulinzi uliimarishwa mjini humo ikiwa ni wiki mbili tangu wanamgambo wa muungano wa mahakama za kiislamu walipotimuliwa Mogadishu na wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia.

Walioshuhudia wamesema rais Yusufu na waziri mkuu Gedi walikwenda katika ikulu ya rais, Villa Somalia, kusini mwa Mogadishu, iliyotumiwa na dikteta Siad Barre kabla kuangushwa madarakani mnamo mwaka wa 1991.