1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu. Mlolongo wa magari ya jeshi la Ethiopia washambuliwa.

Majeshi ya Ethiopia yakiiunga mkono serikali ya Somalia imemuua mtu mmoja na kumjeruhi mwingine leo Jumatatu baada ya mlolongo wa magari yao ya kijeshi kushambuliwa kwa bomu lililotegwa ardhini katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa mlolongo huo wa magari sita ulikuwa unapita katika eneo la kusini la mji huo wakati bomu lililotegwa ardhini lilipolipuka kabla mbele ya gari ya kwanza.

Hakuna taarifa ya mwanajeshi aliyeuwawa ama kujeruhiwa katika shambulio hilo. Majeshi hayo yalifyatua risasi mara baada ya tukio hilo kila upande na kudhibiti eneo hilo kwa muda wa dakika 15 kabla ya kuendelea na safari yao.

Jana Jumapili , bomu lililipuka karibu na magari yaliyokuwa yamemchukua meya wa jiji la Mogadishu na kuuwa kiasi raia wawili .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com