MOGADISHU: Mkutano kupatanisha makundi hasimu Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 13.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Mkutano kupatanisha makundi hasimu Somalia

Zaidi ya wajumbe 1,000 kutoka kila pembe ya Somalia,wanamiminika mji mkuu Mogadishu kuhudhuuria mkutano wa upatanisho uliopangwa kufanywa siku ya Jumapili.Mkutano huo unatazamwa kama ni matarajio ya mwisho ya serikali kuleta amani na kuimarisha mamlaka yake katika nchi hiyo,kwenye Pembe ya Afrika.Lakini kuna matumani madogo ya kupata maendeleo,wakati wanamgambo wa Kiislamu wamekula kiapo kuushambulia mkutano huo. Inaaminiwa kuwa machafuko hayatosita nchini humo,mpaka serikali ya mpito ya Somalia itakapoketi na kuzungumza pamoja na wanamgambo wa Kiislamu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com