1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Marekani yashambulia wanamgambo, Somalia

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvc

Maafisa wa serikali ya Somalia wamesema meli za kivita za Marekani zimekirushia mabomu kijiji kimoja katika eneo lenye milima kaskazini mwa nchi hiyo ambako wanamgambo wa Kiislamu wanasemekana walikuwa wamepiga kambi.

Hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu maafa yaliyosababishwa na shambulio hilo lililotekelezwa jana na manowari ya kimarekani kutokea pwani ya jimbo la Puntland.

Wanamgambo waliokuwa wakilengwa wanaaminika kuwa ni washukiwa wa mtandao wa al-Qaeda waliohusika kwenye mashambulio ya mabomu ya mwaka 1998 kwenye balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania.