1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapambano yazuka tena, 71 wajeruhiwa.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8l

Milio ya makombora na risasi za hapa na pale zimesikika usiku kucha mjini Mogadishu na wakaazi leo Ijumaa wamesema mapigano ya hivi sasa pamoja na shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya kituo cha majeshi ya Ethiopia yameuwa kiasi watu 21 na kuwajeruhi wengine 101.

Wakaazi wa mji huo wamesema kuwa mapigano hayo ambapo kombora moja liliangukia katika soko lililokuwa na watu wengi jana Alhamis , yalikuwa mabaya kama mapambano yaliyochukua muda wa siku nne na kuuwa watu 1,000 mwishoni mwa mwezi wa March na kusababisha karibu asilimia tano ya wakaazi wa mji huo kukimbia.

Daktari mmoja katika hospitali ya Madina amesema kuwa amepokea majeruhi 71 na 41 kati ya hao wako katika hali mbaya na wengine 30 wamepata majeraha madogo madogo.

Mapambano hayo ni kati ya wapiganaji ambao ni kutoka jeshi la mahakama za Kiislamu pamoja na ukoo maafuru katika mji huo wa Hawiye kwa upande mmoja dhidi ya majeshi ya Ethiopia ambayo yanaisaidia serikali ya mpito ya rais Abdullahi Yusuf.