1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Majeshi ya Ethiopia yaondoka Somalia

Majeshi ya Ethiopia yameanza leo kuondoka mjini Mogadishu Somalia, wiki nne baada ya kuwasaidia wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia kuwafurusha wanamamgambo wa mahakama za kiislamu kutoka mjini humo.

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya mpito ya Somalia, Hussein Mohammed Farah Aideed, amesema kikosi cha Umoja wa Afrika kitachukua mahala pa jeshi la Ethiopia katika juma moja lijalo. Hakuna uhakika lakini ikiwa wanajeshi wa Umoja wa Afrika wataweza kuidhibiti hali ndani ya Somalia.

Wakati huo huo, Yemen imekuwa nchi ya kwanza kufungua ubalozi mjini Mogadishu tangu serikali ya mpito ya Somalia ilipofaulu kuwachakaza wanamgambo wa mahakama za kiislamu. Ubalozi huo umefunguliwa katika eneo la K4 kusini mwa Mogadishu.

Balozi wa Yemen nchini Somalia, Ahmed Omar amesema ni heshima kubwa kwa nchi yake kuwa na ubalozi nchini Somalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com