1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Bunge laidhinisha sheria , wasio wabunge kuwa mawaziri.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79E

Wabunge wa Somalia leo wameidhinisha sheria ambayo inaruhusu raia wasio wabunge kuwa mawaziri, wakisafisha njia kwa rais kumteua mtu atakayechukua nafasi ya waziri mkuu Ali Mohammed Gedi aliyejiuzulu mwezi uliopita.

Spika wa bunge la Somalia Sheikh Adan Madobe amewaambia wabunge 200 waliokuwapo bungeni kuwa wabunge wote wameidhinisha mabadiliko hayo, kwa kunyoosha mikono baada ya siku tatu za mjadala.

Ali Mohammed Gedi alijiuzulu siku 10 zilizopita baada ya kutofautiana kwa muda mrefu na rais Abdulahi Yusuf hali ambayo ilidhoofisha serikali katika taifa hilo wakati likipambana na wapiganaji wa muungano wa mahakama za Kiislamu.

Wakati huo huo ghasia katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu zinazuwia huduma za utibabu kuwafikia watu waliojeruhiwa wakati wa mapigano yaliyozuka hivi karibuni, limesema kundi la madaktari wasio na mipaka.