1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jenerali Abdel-Fattah al- Burhani aelekea Uturuki

Saumu Mwasimba
13 Septemba 2023

Mkuu wa majeshi wa Sudan Jenerali Abdel-Fattah al- Burhani ameelekea nchini Uturuki akitafuta kupata uhalali katika mapambano ya kuwania madaraka kati yake na aliyekuwa makamu wake.

https://p.dw.com/p/4WImz

Ofisi ya kiongozi huyo imesema, Al Burhani atafanya mazungumzo na rais Recep Tayyip Erdogan yatakayojikita katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili na njia za kuimarisha mahusiano hayo.

Ziara hiyo imekuja wakati hapo jana mashambulio ya makombora ya wanamgambo wa RSF yaliuwa kiasi watu 17 kaskazini mwa mji mkuu Khartoum,katika eneo la Blue Nile.

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan akutana na kiongozi wa Qatar

Jenerali Al Burhani mpaka sasa ameshazitembelea Misri,Sudan Kusini,Qatar na Eritrea,katika kile ambacho wachambuzi wamekitaja kuwa ni msukumo wa kidiplomasia wa kujiimarisha nafasi yake pale itakapotokea yameitishwa mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.