Mkutano wa pande 4 juu ya Mashariki ya kati | Matukio ya Kisiasa | DW | 31.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa pande 4 juu ya Mashariki ya kati

Mawaziri wa nje wa Marekani,Russia na Ujerumani pamoja wa Umoja wa Ulaya na Katibu mkuu wa UM wamekutana Berlin jana kuzingatia hali ya dharura ya machjafuko huko mashariki ya kati.

Dr..Rice amlahki Bw.Steinmier huko Berlin

Dr..Rice amlahki Bw.Steinmier huko Berlin

Waliokutana ni mawaziri wa nje wa Marekani ,Urusi na Ujerumani pamoja na wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.

Waziri wa nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kwa niaba ya wenzake, alizitaka pande zote zinazogombana kusimamisha ugomvi.Kundi hilo linapanga kikao maalumu mwezi ujao huko huko Mashariki ya Kati.

Kundi hili la pande 4 juu ya mashariki ya kati-Marekani,Russia, UM na UU lina azma ya kuyatilia mkazo matumaini ya kisiasa yaliomo katika ramani ya amani kwa Mashariki ya kati-Road map.Kwa ajili hiyo, wajumbe wa pande hizo 4 watakutana mwezi ujao wa Juni kukutana na Israel na wapalestina pamoja pia na wajumbe wa Arab League-Jumuiya ya Nchi za kiarabu ambao hapo April mwaka huu walianzisha juhudi yao wenyewe ya mashauri ya amani.

“Nadhani kundi la pande 4 juu ya mzozo wa Mashariki ya kati lilijisghulisha zaidi na mzozo huu mnamo nusu mwaka iliopita kuliko wakati wowote kabla tangu mimi kushika wadhifa wa waziri wa nje.”

Katika taarifa yake kundi hilo limetoa mwito kwa pande zote mbili-Israel na wapalestina kurejea katika hali ya utulivu.Likalaani vikali hujuma za makombora yanayofyatuliwa katika ardhi ya Israel na likaitaka Israel nayo kutotumia nguvu kupita kiasi katika hatua zake za kujikinga.

Katibu mkuu wa UM Ban Ki Moon alisema:

“Kukamatwa na Israel kwa wabunge na wajumbe wa serikali wa kipalestina kunazusha wasi wasi mkubwa na tunadai waachwe huru.”

Waziri wa nje wa UU Bibi Benita Ferreo-Waldner alitaja misaada mbali mbali ya kibinadamu inayotolewa kwa raia wa Palestina.

“Na tunakwenda hata zaidi.Kwa kweli, ni azma yetu kutoka hali ya sasa ya kujishughulisha mno na misaada ya dharura, tugeukie ujenzi wa taasisi za kiserikali na miradi ya kimaendeleo.”

Kwahivyo, kuna nia ya pamoja kukomesha hali ya ukosefu wa maendeleo iliopo wakati huu Mashariki ya Kati ingawa pande hizo 4 zinawazindua waliohusika hasa ndio wenye jukumu la kusaka ufumbuzi wa ugomvi wao.

Waziri wa nje wa Russia, Sergej Lvrov, akizungumzia juu ya shehena za silaha zinazokwenda Mashariki ya kati ,alisema ni muhimu kuheshimu makubaliano ya kimataifa juu ya swali hilo na kuzuwia kupeleka huko silaha ambazo zitavuruga hali ya utulivu.

Lavrov aliongeza kusema kuwa wale wanaopeleka silaha Mashariki ya kati wanajua ni silaha za aina gani zinasababisha ukosefu wa utulivu na zipi hazifanyi hivyo.

Mwenzake waziri wa nje wa Marekani Dr.Condoleeza Rice, alihalalisha shehena ya silaha iliopeleka Marekani hivi majuzi kwa jeshi la Lebanon.Aliegemeza hoja yake juu ya azimio la UM lililoitisha Lebanon iwezeshwe kuilinda binafsi mipaka yake.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com