1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mapitio ya Helsinki wafanyika Dar.

24 Novemba 2007

Wawakilishi wa serikali pamoja na vyama vya kijamii kutoka Afrika, Ulaya na maeneo mengine duniani wanakutana kuanzia leo Novemba 27 mjini Dar Es Salaam.

https://p.dw.com/p/CScf

nchini Tanzania, kuangalia masuala ya utandawazi, kuanzia usalama na amani, mazingira na sera za nishati, hadi kuheshimu haki za binadamu , pamoja na utoaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo wa Dar Es Salaam , ambao utafanyika kuanzia Novemba 27 hadi 29, utakuwa wa tatu kufanyika kama sehemu ya hatua za mkutano wa Helsinki wa utandawazi na demokrasia tangu pale ulipoanzishwa mwaka 2002 na serikali za Finland na Tanzania ili kuangalia wasi wasi wa mataifa yanayoendelea kuwa ongezeko la utegemezi wa kimataifa unaleta hali mbaya ya kutokuwa na usawa katika dunia ambayo tayari haina usawa.

Mkutano huo , uliopewa jina la , ushiriki wa utawala , kupunguza mgawanyiko duniani, unafuatia mkutano wa hapo Septemba 2005, uliofanyika nchini Finland katika mji mkuu Helsinki , ukiadhimisha ukamilishaji wa awamu ya kwanza ya hatua hizo.

Jukumu la wadau ambao hawako serikali katika kuhimiza amani na usalama liko juu katika ajenda ya mkutano huo wa mapitio. Nia ya kikao hicho kuhusu amani na usalama ni kuangalia mchango mahsusi wa wale wasio katika serikali unavyowezesha ujenzi wa imani na kuaminiana , changamoto zinazopatikana katika kuendeleza demokrasia na usalama katika mazingira yasiyokuwa salama, na uwezekano wa wadau ambao hawako serikali kuchangia katika kutatua mizozo, hususan mashariki ya kati, amesema Folke Sundaman , kutoka wizara ya mambo ya kigeni ya Finland. Mada nyingine itakayojadiliwa kwa urefu mjini Dar Es Salaam ni uhusiano baina ya sera za kiuchumi za kitaifa na dunia kwa jumla.

Lengo la mjadala huu utakaofanyika mjini Dar Es Salaam ni kuangalia vipi nchi zinazoendelea zinaweza kutumia vizuri sera zao zilizopo na kufaidika zaidi katika misingi ya uchumi wa dunia, amesisitiza Sundman. Vipi mfumo wa uchumi wa dunia unaweza kwa vizuri zaidi kusaidia mipango ya maendeleo ya kitaifa, na hatua gani za ubunifu pamoja na njia mpya za ushirikiano baina ya wadau mbali mbali zinaweza kutaamali au kufikiriwa katika kiwango cha kitaifa na dunia, hayo yote yatajadiliwa kwa mujibu wa Sundman.

Katika mkutano wa Helsinki , iliamuliwa kuwa hatua hizi, zinazorahisishwa na ushiriki wa serikali za Tanzania na Finland , zinapaswa kuendelea na kazi ya kuhamasisha dhamira ya kisiasa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya kidunia na uendelezaji wa ushiriki wa wadau wengi zaidi katika utawala wa dunia, Ilkka Kanerva , waziri wa masuala ya kigeni wa Finland , amesema katika azimio la pamoja na mwenzake wa tanzania Bernard Membe.

Dhana ya kuwa na ushirikiano wa wadau wengi zaidi uko katika msingi wa kukubali kuwa utandawazi umeleta mabadiliko ya kimsingi katika siasa za dunia, mataifa, ambayo yalizoeleka kuonekana kama yenye haki ya utendaji katika medani ya kimataifa , yameunganishwa na wadau wengine, kama vile mashirika ya kimataifa, mashirika ya vyama vya kijamii , na biashara na wadau wa kidini.