1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kukabiliana na taka za plastiki waanza Ottawa

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Duru ya nne ya mazungumzo ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki duniani inaanza leo mjini Ottawa nchini Canada.

https://p.dw.com/p/4f6MI
Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 170 duniani wanatarajiwa kushiriki mazungumzo ya taka za mifuko ya plastiki
Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 170 duniani wanatarajiwa kushiriki mazungumzo ya taka za mifuko ya plastikiPicha: Johannes Panji Christo/Anadolu/picture alliance

Shinikizo linaongezeka kwa wajumbe kufikia rasimu ya makubaliano kabla ya duru ya mwisho ya mazungumzo nchini Korea Kusini mwezi Disemba.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ziliweka shabaha ya kuafikiana juu ya mkataba wa kimataifa ifikapo mwisho wa mwaka huu. Lakini mkutano wa awali uliofanyika Kenya mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita haukupata mafanikio makubwa.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, tani zipatazo bilioni 9.2 za plastiki zimezalishwa tangu mwaka 1950. Idadi kubwa ya taka hizo haziwezi kuoza na hivyo kuishia kurundikana baharini na mitaani.