1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa juu ya kupiga marufuku mabomu ya mtawanyiko waanza leo mjini Oslo Norway

22 Februari 2007

Wajumbe kutoka nchi 40 leo wameanza mkutano wa siku mbili mjini Oslo nchiniNorway kujadili haja ya kuunga mkono hatua ya kupiga marufuku mabomu ya mtawanyiko yanayosababisha vifo vya maalfu ya watu katika sehemu za mizozo.

https://p.dw.com/p/CHJX

Lengo la kupiga marufuku silaha hizo sasa zinaungwa mkono pia na maseneta mawili wa chama cha demokratik cha Marekani.

Marekani ni miongoni mwa nchi zinazounda mabomu hayo na kuuza kwa nchi zingine. Kwa sasa Marekani ina kiasi cha mabomu milioni tano na nusu ya aina hiyo katika maghala yake ya silaha.

Mabomu hayo yalitumiwa katika vita vya ghuba mnamo mwaka 1991, pia yalitumika katika vita vya Kosovo, Afghanistan na sasa nchini Irak.

Umoja wa Mataifa umekadiria kwamba kuna mabomu hayo ya mtandazo katika nchi zaidi ya 20 yanayofikia idadi alfu 33 ambayo bado hayajaripuka.

Mwaharakati wa kutetea haki za binadamu bwana Steve Goose ameeleza kuwa mabomu hayo husambaa kiasi cha eneo lenye ukubwa wa uwanja wa mpira na wakati mwingine huenea katika eneo kubwa zaidi na mara nyingine hayaripuki kama inavyokusudiwa. Hivyo basi huendelea kuzagaa kama mabomu ya kutegwa chini ya ardhi.

Wataalamu wanasema kuwa ili kuripuka silaha hizo hazihitaji mtu kuzikanyaga. Uepo tu unatosha kusababisha maradha makubwa.

Mabomu hayo yameundwa ili kuweza kuua idadi kubwa ya askari wa miguu ama kuwajeruhi.

Lakini hadi sasa asilimia 98 ya watu waliodhurika na silaha hizo ni raia na hasa watoto. Mfano wa hivi karibuni ni Lebanon ambako majeshi ya Israel yalitumia mabomu hayo.

Kama muundaji na mtumiaji mkubwa wa silaha hizo Marekanai siku zote imekuwa inapinga kuzungumzia juu ya silaha hizo. Lakini maseneta wa chama cha demokratik hivi karirbu n waliwasilisha mswada wa sheria juu ya kudhibiti matumizi na uuzaji wa mabomu ya aina hiyo.

Miongoni mwa nchi zinazopinga mazungumzo yoyote juu silaha hizo ni pamoja na China, India,Pakistan Urusi na Uingereza.

Mkutano unaofanyika mjini Oslo leo una lengo la kupiga marufuku silaha hizo.

Watetea haki za binadamu wanasema kwamba ikiwa hatua hiyo ya kupiga marufufku itafikiwa, maisha ya maalfu ya watu na hasa ya watoto yataokolewa.