1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa juu ya Irak

3 Mei 2007

Waziri Mkuu wa Irak Nouri al -Maliki ameitaka jumuiya ya kimataifa iifutie madeni nchi yake. Bwana al Maliki ametoa mwito huo kwenye mkutano wa kimataifa unaofanyika nchini Misri juu ya kuleta amani na kujenga upya uchumi wa Irak.

https://p.dw.com/p/CHEs
Waziri Mkuu wa Irak Nouri al-Maliki
Waziri Mkuu wa Irak Nouri al-MalikiPicha: AP

Akizungumza kwenye mkutano huo wa kimataifa uloanza leo katika kitongoji cha mapumziko,Sharm el Sheikh kwenye bahari ya Sham nchini Misri waziri mkuu wa Irak bwana al Maliki pia ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa juu ya kuwaunga mkono watu wa Irak katika juhudi za kujenga umoja wa nchi yao.Amesema Irak inahitaji fedha ili kuziekeza katika miradi ya kujijenga upya .

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kuwa nchi yake ipo tayari kufuta sehemu fulani tu ya deni la Irak Hapo awali kulikuwa na habari kwamba Saudi Arabia ilikuwa tayari kufuta hadi asilimia 80 ya deni la dola bilioni 17.

Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi tajiri na jirani wa Irak.Pamoja na wajumbe hao ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice anaetarajiwa kukutana na wawakilishi wa Iran na Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank-Walter Steinmeier pia anahuduria mkutano huo .

AM.