1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa G-8

25 Mei 2007

Kati ya Juni 6-8 utafanyika mkutano wa kilele wa kundi la G-8-dola kuu 8 za kiviwanda ulimwenguni huko Heilgendam,Ujerumani. Afrika na jinsi ya kuongezewa misaada ilioahidiwa ni mojawapo ya mada kuu.

https://p.dw.com/p/CHko

Zikiwa zimesalia wiki 2 kabla kuanza kwa mkutano wa kilele wa kundi la dola kuu 8 tajiri ulimwenguni-G-8,kuheshimiwa haki za waandamanaji na kutimizwa ahadi za nchi hizo za viwanda kwa bara la Afrika, ni maswali yalio shinani mwa maandalio ya mkutano huo wa kilele utakaofanyika nchini Ujerumani.

Kanzela angela Merkel wa Ujerumani Mei 22, alitoa ahadi kuwa kundi la G-8 litatekeleza ahadi kadhaa lililotoa kwa bara la afrika.

“Tunapaswa kuonesha uaminifu wetu na kweza kwetu kutegemewa.” Alinukuliwa Kanzela Merkel kusema hapo juzi huko Berlin wakati wa Jukwaa la 8 la ushirika na Afrika .

Jukwaa hilo lililoasisiwa na Shirika la ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo (OECD),Banki kuu ya Dunia na nchi za kiafrika zilizounda Ushirika mpya kwa maendeleo ya Afrika (NEPAD), lilijadili upande wa kiuchumi,kisiasa na kijamii wa maendeleo.

Kanzela wa Ujerumani lakini, hakufikia umbali wa kuhakikisha kwamba mkutano ujao wa kilele wa kundi la dola kuu 8-G-8 nchini mwake utaongeza misaada maradufu kwa afrika hadi ifikapo 2010 kama ilivyoahidiwa na kundi hilo wakati wa mkutano wa kilele wa Gleneagles,Scotland.

Badala yake, Kanzela Merkel alisisitiza juu ya fursa za ukezaji wa makampuni ya kibinafsi zinazoongezeka barani Afrika.

“Yeyote yule ataketia raslimali zake barani afrika hii leo,atakuja kuvuna matunda yake hapo kesho.”alisema Kanzela Merkel.

Akaongeza na ninamnukulu, “Afrika ni bara lenye fursa kubwa mno za kutia raslimali.”

Kundi la dola kuu 8 za kiviwanda linajumuisha Uingereza,Kanada,Ujerumani,Ufaransa,Itali,japan,Russia na Marekani.Linakutana kati ya juni 6-8 katika mji uliopo kandoni mwa pwani ya Baltik wa Heiligendamm.

Mbali na mada ya misaada kwa Afrika,kundi hilo limeingiza katika ajenda yake maswali kama utulivu wa masoko ya fedhaulimwenguni,mfumo wa biashara duniani na sera ya kimataifa ya kupiga vita kuzidi kwa hali ya ujotoduniani.

Kabla ya Jukwaa la ushirika na Afrika kufanyika huko Berlin, mawaziri wa fedha na wa kiuchumi wa kundi hili la G-8, walikutana hapo mei 19 mjini Potsdam,km kiasi 20 hivi kusini mwa Berlin.Katika azimio lao walisema na ninanukulu,

“Tunahakikisha tena nia yetu ya kutimioza ahadi tulizotoa kama wafadhili na hasa katika kutoa misaada kwa Afrika.”

Lakini kwa muujibu wa nakala isio rasmi ya tangazo lililotungwa na serikali ya Ujerumani kwa ajili ya mkutano wsa Heiligendamm, dola kuu hizo 8 zitaahidi kuongeza msaada rasmi wa maaendeleo kwa Afrika kwa kima cha dala bilioni 25 kila mwaka hadi ifikapo 2010-hiki ni kima kidogo sana kutoka kile cha dala bilioni 67 kwa mwaka, kilichoahidiwa wakati wa kikao cha Gleneagles,huko Scotland 2005.