Mkutano wa IOC wafanyika mjini Kampala,Uganda
25 Januari 2010Matangazo
Mbali na suala la ugaidi, mkutano huo pia unapania kutafuta mkakati wa kuboresha umoja na upatanishi katika nchi wanachama. Kuimarishwa kwa elimu na kudhibiti hali ya usalama katika mataifa hayo ni miongoni mwa mada ambazo pia zitakuwa mezani. Wawakilishi katika mkutano huo wanatokea Mashariki ya Kati, Bara la Asia, Afrika na hata nchi za eneo la Balkan, barani Ulaya. Mkutano huo ulioanza jana utamalizika tarehe 31.
Leyla Ndinda kutoka Kampala ana ripoti kamili.
Mtayarishaji: Leyla Ndinda
Mhariri: Othman Miraji