1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa AU waanza

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanaanza kikao chao leo Jumapili (15.07.2012) ambacho kitashughulikia masuala mawili muhimu katika bara hilo.Uchagua wa rais wa halmashauri kuu huenda ukagubika agenda za mkutano huo.

epa03304375 This hand out image dated 12 July 2012 shows South African Minister of International Relations and Cooperation, Ms Maite Nkoana-Mashabane, at the Executive Ministerial Meeting of the AU, Addis Ababa, Ethiopia, 12 July 2012. EPA/Jacoline Prinsloo/HO +++(c) dpa - Bildfunk+++

Mkutano wa AU mjini Addis Ababa

Nkosazana Dlamini-Zuma kutoka Afrika kusini atapambana na rais wa sasa wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika , Jean Ping, baada ya wawili hao kushindwa kupata theluthi mbili ya kura zinazotakiwa katika mkutano uliopita , na kumuacha Ping katika wadhifa huo kwa miezi sita mingine. Watapambana tena leo wakiwania wadhifa huo, ambao Ping ameushikilia tangu mwaka 2008.

Wagombea wote wametoa taarifa kali kabla ya uchaguzi huo wa Jumapili. Mapema wiki hii , Ping alikanusha ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari vya Afrika kusini kuwa atajitoa katika kinyang'anyiro hicho kumruhusu Dlamini -Zuma kugombea bila kupingwa, na kusababisha jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC kumshutumu Ping kwa kutumia vibaya mali za Umoja wa Afrika katika hatua za kuelekea katika uchaguzi huo.

African Union Commission chairman Jean Ping arrives for the 18th African Union (AU) Summit in the Ethiopia's capital Addis Ababa, January 29, 2012. REUTERS/Noor Khamis (ETHIOPIA - Tags: POLITICS HEADSHOT)

Rais wa halmashauri ya umoja wa Afrika Jean Ping

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema utamaduni uliopo ni kwamba mataifa makubwa katika bara hilo hayajiingizi katika kuwania wadhifa wa rais wa halmashauri ya umoja huo, na kuyaachia mataifa madogo kuchukua wadhifa huo, na uamuzi wa Afrika kusini kukiuka sheria hiyo ambayo si rasmi imezusha hisia mbaya.

Die Außenministerin der Republik Südafrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, gibt am Montag (09.03.2009) ein Kurzstatement im Auswärtigen Amt in Berlin. Zuvor führte sie ein Gespräch mit Bundesaußenminister Steinmeier (SPD) zu aktuellen internationalen und afrikapolitischen Themen, wie die Lage in Simbabwe. Foto: Arno Burgi dpa +++(c) dpa - Report+++

Nkosazana Dlamini- Zuma, anayewania wadhifa wa urais wa halmashauri kuu ya AU

Ping huenda akabakia rais

Iwapo itashindikana kumshagua rais wa halmashauri hiyo mara hii, Ping anaweza kisheria kubaki madarakani kama kiongozi hadi mkutano ujao Januari 2013.

Masuala ya kiusalama pia yanapewa umbele katika mkutano huo, huku viongozi wakiangalia zaidi kuhusu hali isiyo thabiti nchini Mali, ghasia zilizozuka tena katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na mzozo unaoendelea kati ya Sudan na Sudan kusini.

(FILE) A file picture dated 19 January 2010 shows Sudanese President Omar el Bashir (R) and First Vice President and President of the Government of Southern Sudan, Salva Kiir Mayardit (L), participating in celebrations marking the 5th anniversary of the signing of the Comprehensive Peace Agreement (CPA) in Yambio, Sudan. Omar el Bashir has won the country's first multiparty elections in 24 years, election officials said on 26 April 2010. The polls are supposed to usher in a new era of democracy in Sudan, which is recovering from a decades-long civil war between the north and south. EPA/TIM MCKULKA - UNMIS - HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++

Marais Omar el Bashir na Salva Kiir Mayardit wa Sudan na Sudan kusini walikutana mjini Addis Ababa

Kufuatia mkutano wa baraza la usalama na amani la umoja huo Jumamosi, umoja wa Afrika umetaka kukomeshwa kwa kile ulichokiita , uingiliaji kati usiokubalika, unaofanywa na uongozi wa zamani wa kijeshi nchini Mali kufuatia mapinduzi hapo Machi mwaka huu na kutoa wito wa kuvunjwa kwa utawala huo wa zamani wa kijeshi.

Congo na Rwanda kujadiliwa

Tawi la usalama la umoja huo wa Afrika pia limeitisha mkutano wa ngazi ya viongozi wa nchi kwa mataifa ya kieneo kutafuta suluhisho la ghasia zinazoongezeka mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Baraza hilo la usalama limehimiza kupatikana kwa suluhisho la haraka katika mizozo iliyopo kati ya Sudan na Sudan kusini mwishoni mwa mkutano wa usalama , ambao ulihudhuriwa na rais wa Sudan Omar al-Bashir na mwenzake wa Sudan kusini Salva Kiir.

Viongozi hao wa Sudan na Sudan kusini ambao nchi zao zilikaribia kupigana vita , walikutana Jumamosi kwa mara ya kwanza kwa mazungumzo ya faragha tangu kuzuka kwa mapigano.

Mkutano huo wa umoja wa Afrika unakwenda kwa kauli mbiu ya kuimarisha biashara baina ya mataifa ya Afrika, kama ilivyokuwa katika mkutano wa Januari wa umoja huo. Maafisa wanasema wameamua kuweka mada moja kila mwaka badala ya mada mpya katika kila kikao, kama ilivyokuwa hapo zamani.

Mkutano huo unafanyika katika mji mkuu wa Ethiopia , Addis Ababa baada ya rais mpya wa Malawi Joyce Banda kukataa kumwalika Bashir, ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita na madai ya mauaji ya kimbari.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Idd Ismail Ssesanga

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com