1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mdogo wa viongozi wa Ulaya mjini Sintra

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2o

LISSABON:

Kansela Angela Merkel yuko ziarani nchini Ureno kwa mashauriano kuhusu katiba ya Umoja wa ulaya.Katika mkutano huo unaofanyika katika muji mdogo wa Sintra,magharibi ya mji mkuu wa Ureno-Lisabon,wanashiriki pia viongozi wa serikali za Ureno na Slovenia na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya.Ureno na Slovania ndizo zitakazoshika,zamu ya mwenyekiti wa Ulaya,baada ya Ujerumani,kuanzia nusu ya pili ya mwaka huu .Mada kuu katika mazungumzo ya Sintra ni mustakbal wa katiba ya Umoja wa ulaya.Kansela Angela Merkel angependelea kuwasilisha pendekezo jipya,mkutano wa viongozi wa umoja wa ulaya utakapoitishwa mjini Bruxells wiki sita kutoka sasa.Katiba mpya ya Umoja wa Ulaya imekwama tangu ilipokataliwa na wapiga kura wa Ufaransa na uholanzi.