Mkutano kuhusu Ugonjwa wa Malale wafanyika mjini Kampala
21 Septemba 2009Matangazo
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi kubwa ya
wakaazi barani Afrika wanaugua ugonjwa wa malale wengi wao
wakiwa kwenye maeneo ambayo yamo karibu na wanyama pori au
kwenye jamii za wafugaji. Wataalam wa ugonjwa huo, wanasayansi,
wanasiasa na mashirika ya kimataifa walikutana hii leo mjini
Kampala nchini Uganda kujadili ni vipi watakavyokabiliana na
changamoto za ugonjwa huo na hukakikisha unasahaulika barani
Afrika. Mwandishi wetu mjini Kampala, Leylah Ndinda anaripoti zaidi.
Mpitiaji: Grace Patricia Kabogo
Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman