1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu mgogoro wa Darfur

P.Martin27 Oktoba 2007

Wajumbe wamekusanyika mji wa Sirte nchini Libya kuzindua majadiliano yanayolenga kumaliza mgogoro wa miaka minne na nusu katika jimbo la Sudan, Darfur.

https://p.dw.com/p/C77S

Lakini kuna shaka ikiwa mkutano huo utaweza kupata makubaliano ya maana,kwa sababu makundi makuu mawili ya waasi yamesusia mazungumzo hayo ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Makundi hayo mawili ni Kundi la Haki na Usawa JEM na Umoja wa jeshi la Ukombozi wa Sudan SLA-Unity. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Jan Eliasson aliesaidia kutayarisha mkutano huo wa amani amesema,ni matumaini yake kuwa wataweza kuyashawishi makundi hayo mawili kuhudhuria mkutano huo.