1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkasa wa kuzama kwa meli Zanzibar: Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya uzembe

12 Septemba 2011

Huku kikosi cha wazamiaji na meli ya uzamuaji kutoka Afrika ya Kusini kikiwasili Zanzibar kuizamua meli ya Mv Spice Islander, serikali inasema itachukua hatua kali dhidi ya uzembe ikiwa utabainika.

https://p.dw.com/p/12XGo
Miongoni mwa watoto walionusurika kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islander nchin Zanzibar hapo Jumamosi ya Septemba 10, 2011.
Miongoni mwa watoto walionusurika kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islander nchin Zanzibar hapo Jumamosi ya Septemba 10, 2011.Picha: picture-alliance/dpa

Kikosi cha wazamiaji 12 kutoka Afrika Kusini ´kimewasili visiwani Zanzibar kusaidia kutafuta maiti za watu takriban 200 waliozama ndani ya meli mapema Jumamosi iliyopita. Matumaini ya kuweza kuwaokoa watu zaidi kufuatia ajali ya meli huko Zanzibar yamefifia.

Wakati huo huo, serikali ya Zanzibar imeapa kwamba itachukuwa hatua zinazostahiki kwa wale wote watakaobainika kufanya uzembe katika mkasa wa kuzama kwa meli hii.

Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman