1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa China azuru New Delhi

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTK

BEIJING:

India imemualika mjumbe wa hadhi ya juu wa chama cha kikoministi cha jamhuri ya Watu wa china ambae yamkini akawasili na risala ya kisiasa kutoka uongozi wa China juu ya wasi wasi wa jirani yake huyo kwa mapatano ya ushirikiano wa kinuklia ambao India imefunga na Marekani.

Akiitikia mualiko wa wizara ya nje ya India,katibu-mkuu wa chama cha kikoministi Wang Yang atafunga safari ya wiki moja ya kirafiki nchini India.