Mji wa Pyeongchang kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympics 2018 | Michezo | DW | 07.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Mji wa Pyeongchang kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympics 2018

Wakorea kusini usiku wa kuamkia leo wamesherehekea kwa kurusha fataki angani, baada ya nchi hiyo kutangazwa rasmi kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympic ya majira ya baridi mwaka 2018.

default

Mkuu wa kamati ya Kimataifa ya Olympic Jacques Rogge, akiutangaza mji wa Pyeongchang

Mji wa Pyeongchang, umeshinda zabuni kwa kauli mbiu ya "upeo wa fikra mpya'', baada ya kupata ushindi wa kura nyingi dhidi ya miji mingine iliyokuwa ikiigombea nafasi hiyo, Munich wa Ujerumani na mji wa Annecy wa Ufaransa, kutoka katika kamati ya Kimataifa ya Olympic.

Südkorea Olympische Spiele Pyeongchang 2018

Rais wa Korea ya Kusini Lee Myung-bak (katikati) akisherehekea pamoja na wajumbe wengine

Awali akizungumzia ushindi huo wa Korea kusini, Rais wa kamati ya Kimataifa ya Olympic Jacques Rogge amesema ushindi huo mkubwa uliopata mji wa Pyeongchang, katika awamu ya kwanza ya uchaguzi, umemshangaza hata yeye binafsi.

 • Tarehe 07.07.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11qdn
 • Tarehe 07.07.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11qdn