Mjerumani aliuliwa kwa kupigwa risasi sita. | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mjerumani aliuliwa kwa kupigwa risasi sita.

Wakati serikali ya Ujerumani inafanya juhudi za kumkomboa mwananchi wake, mhandisi , alietekwa nyara nchini Afghanistan ,uchunguzi umethibitisha kwamba mjerumani mwengine alietekwa nyara pamoja na mhandisi huyo aliuawa kwa kupigwa risasi.

Frank-Walter Steinmeier

Frank-Walter Steinmeier

Mjerumani huyo aliekuwa na umri wa miaka 44 alitekwa nyara mwezi jana pamoja na mjerumani mwingine katika jimbo la kati la Afghanistan Maidan Wardak.Uchunguzi uliofanywa na madaktari umeonesha kwamba mtu huyo alipigwa risasi kichwani.

Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya nje bwana Martin Jäger ameeleza kuwa uchunguzi umeonesha kwamba mjerumani huyo ambae pia alikuwa mhandisi alizirai kabla ya kupigwa risasi sita.

Wakati huo huo serikali ya Ujerumani imeimarisha juhudi ili kuokoa maisha ya mjerumani mwengine ambae bado yumo katika mikono ya wateka nyara nchini Afghanistan.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank - Walter Steinmeier amesema juhudi zote sasa zitaelekezwa katika kumkomboa mjerumani huyo.

AM.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com