Mizozo ya Sudan itatuliwe kwa amani
24 Juni 2011Matangazo
Sudan Kusini inatazamia kutangaza uhuru wake Julai 9, wakati ambapo Ujerumani itakuwa na wadhifa wa urais katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pande hizo mbili za Sudan zinakabiliwa na mizozo kadha ya mipaka.
Hata hivyo, zimekubaliana kuwa na eneo ambako majeshi hayatoruhusiwa katika jimbo hilo la mpakani la Abyei. Migogoro mingine inayohitaji kutenzuliwa inahusika na ugawaji wa pato la mafuta pamoja na njia ya kugawana madeni ya taifa. Waziri Westerwelle leo anatazamiwa kwenda Sudan Kusini kukutana na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mjini Juba.