Mitumba kupigwa marufuku Kenya | Masuala ya Jamii | DW | 02.03.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mitumba kupigwa marufuku Kenya

Serikali ya Kenya inakusudia kuzuia uingizaji wa mitumba nchini humo kutokana na nguo hizo kuukuu kusababisha viwanda vya nguo mpya vya ndani kukosa soko.

default

Soko la Mitumba Nairobi

Katibu Mkuu wa viwanda nchini humo Kibicho Karanja ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mafundi Mchundo katika Mji wa Thika nchini humo. Huku kauli hii ikiwaudhi raia Kenya ambao ni wateja wa mitumba

“Ikiwa mitumba haitakuja Kenya, basi vijana wengi watakosa kazi alafu watu kujikimu kimaisha itakuwa kazi.“ walisema baadhi ya raia wa nchi hiyo.

Kwanza kabisa Wafanyabiashara nchini Kenya walishuhudia serikali yao ikipandisha kodi kwa nguo hizo kukuku. Kumekuwa na sababu kadhaa juu ya biashara ya mitumba kwa mataifa ya Afrika.

“Toka Novemba waliongoza asilimia ishirini na sasa asimilia Ishirini moja, tukawauliza wakasema juu ya kodi“ anasema raia anayelalamikia kodi

Kupandisha huko kwa kodi kuliibua malalamiko mengi si kwa raia huyo tu hata wanawake kadhaa ambao wanaofanya biashara hiyo katika maeneo mengi katika taifa hili lililopo Afrika ya Mashariki.

Bidhaa hii ambayo ni maarufu sana Afrika ya Mashariki ambayo iliingia kwa mara ya kwanza miaka ya 1980 ikiwa na jina la KAFA ULAYA MAZISHI AFRIKA ilipata mwanya huo kwani palikuwa na matatizo katika viwanda vya nguo ukanda huo wa Afrika na madhara yake yakaonekana miaka ya 1990 mara baada ya viwanda hivyo vya nguo kufa kabisa.

Ushuhuda wa hili unaoneka hasa kwa sasa kwani viwanda vya nguo vya Kenya vinawapa ajira watu chini ya 20,000 tu. Wakati ajira za awali zilifikia 200,000 wakati viwanda vya nguo vilikuwa vimeshamiri.

Jaswinder Bedi ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wazalishaji nchini humo anaunga mkono kuwa mitumba ndiyo iliyosababisha athari kubwa kwa viwanda vya nguo nchini Kenya.

Anasema hauwezi kushindana kwenye biashara na bidhaa ambayo haina kodi. Kwani wao wana jukumu la gharama za uzalishaji, na jukumu la kununua malighafi. Ni vigumu kushindana. Bidhaa hii ambayo inatoka nchi za magharibi inaingia mara baada ya kukusanywa na makampuni yanayofanya kazi za kuzitengeneza upya mara baada ya matumizi. Baada ya kufanya hivyo hufungwa kwenye marobota na kupelekwa katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo kuna wateja wengi.

“Ninaziuza sokoni nguo zangu kuukuu ambazo sizihitaji. Zile ambazo haziuziki ninazitupa. Ninatumai zinawasaidia watu ambao hawawezi kununua nguo mpya. Hasa watu wa mataifa masikini.” Anasema raia mmoja nchini ujerumani.

Sally Bade na Catherine Barber walifanya utafiti juu ya tatizo hili la mitumba katika andiko lao juu ya madhara ya mitumba katika mataifa yanayoendelea chini ya udhamini wa Oxfam.

Wanabainisha kuwa kwa mwaka mmoja Mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la sahara yanatumia zaidi dola bilioni 1 kwa ununuzi wa mitumba huku nchi ya Senegal pekee kwa 1996 walinunua nguo hizo zaidi ya milioni nane huku nguo mpya milioni tano tu.

Inaaminika kuwa kama Serikali ya Kenya itazuia uingizaji wa nguo hizo unaweza kupunguza ajira nyingi kwa raia wake. Hasa kwa wale wanazozisambaza, kwenye masoko, wale wanaokarabati, wale wanaotengeneza kwenye mitindo mipya na hata wale wanaozifua na wale wauzaji.

Huku masoko kadhaa ya bidhaa hizo katika nchini za Afrika Mashariki kama vile Mwembe Tayari na Mwembe Kuku kwa Mombasa, River Rori huko Nairobi nchini Kenya Karikoo, Tandika jijini Dar es Salaam na Kibororoloni huko Moshi kwa Tanzania yaliweza kushamiri na kuwa na umaarufu kwa bishaara hii kwa muda mrefu.

Mwandishi :Adeladius Makwega
Mhariri:Josephat Charo