Misri yaongoza katika All-Africa Games | Michezo | DW | 23.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Misri yaongoza katika All-Africa Games

Michezo ya bara la Afrika inamalizika leo huko Algiers huku Misri ikiongoza tena katika orodha ya medali ikifuatwa na wenyeji-Algeria.Kenya na Ethiopia zatamba katika riadha.

Simba wa nyika-Kamerun wametangaza kuwa wanasaka kocha mpya licha ya kuwa kocha wake wa sasa kutoka nyumbani Jules Nyongha,amezinyonga timu zote ambazo zilikumbana na simba wa nyika kuania tiketi za finali ya kombe la Afrika mwakani nchin I Ghana.

Shirikisho la dimba la Kamerun limetangaza kuwa linamsaka kocha mpya katika mtandao wao na hii ina maana enzi ya kocha Nyongah imemalizika.Nyongha,akiungwamkono na staid wa Kamerun, Samuel Eto’o .Nyongha, amepokonywa ukocha mwezi tu baada ya kuipatia Kamerun tiketi ya kwenda Ghana,mwakani kunguruma katika kombe la Afrika.

Sasa shirikisho la dimba la Kamerun linakaribisha maombi hadi August 6.Inasemekana hatahivyo, kocha wa kibelgiji George Heylens yuko usoni kushika wadhifa huo baada ya mazungumzo yake aliofanya na wakuuwa wizara ya michezo mjini Yaounde.

Kura ya kuzikutanisha timu 16 za finali ya kombe la Afrika la mataifa januari mwakani huko Ghana, sasa itapigwa Okotoba 19.

Wenyeji Ghana waingia bilakupingwa.Angola,Kamerun,Morocco,Nigeria,Sudan na Tunisia, tayari nazo zimeshatia kibindoni tiketi zao.Changamoto za mwisho kwa timu zilizobakia zitakuwa mwishoni wa wiki ya mwisho kabla kura hiyo kupigwa.Katika kombe hilo la afrika, mechi zitachezwa Accra,mji mkuu,Kumasi,Sekondi na Tamale.

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani afrika ,mabingwa mara 5 Al Ahly ya Misri,wameizaba Esperence ya Tunisia mjini Cairo mabao 3-0-shukurani kwa mabao ya Aboutraika,muangola Falivio Amado na Osama Hosny.

Ama katika kinyan’ganyiro cha kombe la shirikisho la dimba la Afrika,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ilitoka nyuma na kuizaba TP mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo mabao 3-2.

Club Sportif Sfaxien ya Tunisia , iliondoka suluhu bao 1:1 na Astres Douala ya Kamerun.

Katika Kombe la Asia,Saudi Arabia ilivuka salama-usalimini kutomezwa na Uzbekistan na m,wishoe ikaondoka na ushindi wa mabao 2-1.

Sasa inakutana na Japan katika nusu-finali.

Irak pia imekata tiketi ya nusu-finali ya kombe hilo na huko Baghjdad ilikua shamra-shamra licha ya hofu za usalama.Irak iliilaza Vietnam mabao 2:0.Mashabiki wa kisunni na wa kishia walishirikiana kuangalia dimba na kusherehekea ushindi.

Timu za kanda ya Afrika mashariki zinajiwinda kwa kuanza kwa kinyan’gabnyiro cha kombe la tusker mwishoni mwa wiki hii wakati timu ya taifa ya Zanzibar-Zanzibar Heroes imefunga safari ya 3 mnamo miaka 3 mfululizo kuja Ujerumani:

Katika All-Africa -Games michezo ya bara la Afrika inayomalizika leo mjini Algiers,Tanzania inarudi nyumbani ikiwa ina medali 1 tu ya fedha.

Kenya,kinyume na Tanzania imetamba,lakini sio kifua mbele kwani, waethiopia mahasimu wao katika riadha,waliwatoa jasho:Misri imeibuka kileleni kiongoza kwa medali za dhahabu,fedha na shaba ikifuatwa na wenyeji Algeria huku Afrika Kusini ikikamata nafasi ya tu.Nigeria, ilibidi kuridhika na nafasi ya 4.

 • Tarehe 23.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbc
 • Tarehe 23.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbc