Miripuko yaua watu 72 Baghdad | Michezo | DW | 01.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Miripuko yaua watu 72 Baghdad

Hali ya wasi wasi imerudi Baghdad baada ya miripuko 2 ya mabomu kuua hadi watu 72.

Miripuko 2 ya bomu yaliteketeza soko maarufu mjini Baghdad leo na kusababisha vifo vya watu 72-idadi kubwa ya wahanga tangu kupita miezi 6.Shambulio hili la leo lni pigo kali kwa juhudi za kurejesha usalama nchini Iraq.

Polisi imearifu mwanamke aliejiripua aliua watu 45 na kuwajeruhi wengine 82 sokoni kati-kati ya jiji la Baghdad.Mripuko mwengine wa bomu muda mfupi baadae uliua watu wengine 27 na kuwajeruhi 67 katika soko la kuuza ndege kusini mwa baghdad.

Ramadhan Ali na taarifa zaidi:

Katika soko la Ghazil,mojawapo ya mahala mashuhuri pa kukusanyika watu mjini Baghdad na palipohujumiwa mara tatu mwaka jana,watu wakiangalia kilichopita hapo hii leo na mateketezo huku wafanyikazi wakikusanya maiti na viungo vya wanadamu na masanduku ya wanyama yaliochururika damu.

Shahidi mmoja amesema mwanamke mmoja aliejiripua kwa bomu aliingia sokoni akidai ana ndege anaotaka kuuza.Jumla ya watu wakajikusanya na akalifyatua bomu kutoka mavazi yake.Polisi imearifu bomu la pili lililikua lililoegeshwsa kandoni mwa barabara.

Meja-jenerali Qassim Moussawi,msemaji wa Jeshi la Iraq mjini Baghdad amesema katika hujuma zote mbili wanwake 2 walivaa mabomu ambayo yaliripuliwa kutoka mbali.“Tumegundua simu zilizotumika kuwaripua wanawake hao.“ Alisema Jenerali moussawi.

Polisi na maafisa wsa ulinzi wa raia wakawakusanya waliojeruhiwa n a kuwatia katika mikokoteni ,kwenye motokaa na kwenye malori huku wanajeshi wa kimarekani wakisaidia kuweka ulinzi katika eneo hilo.

Soko hilila wanyama la Ghazil hufunguliwa kila ijumaa tu na linapendwa sana kutembelewa na wakaazi wa baghdad.Linauza aina mbali mbali ya wanyama wenye rangi tofauti na za kupendeza –kuanzia mbwa wa kulinda majumba ,nyani hata kasuku na njiwa.Hata samaki wa nchi za joto wanapatikana hapo.

Hujuma ya bomu iliofanyika Novemba mwaka jana ilisababishwa na bomu lililofichwa ndani ya boxi lililokuwa na ndege.Hii ilisababisha hofu vichwani mwa wakaazi wa jiji la baghdad walioanza kurtejea kuzowea hali ya zamani ya usalama .katika juma zilizopita, watu 10 waliuwawa hapo.Hujuma ya leo ndio mbaya kabisa kutokea Baghdad tangu kupita miezi 6.

Machafuko yalipungua nchini Iraq kwa kima cha hadi 60% tangu juni mwaka jana hali ambayo iliwaruhusu wairaqi kujasiri kwenda masokoni na mikahawani kurejea kuishi kikawaida.

Kupungua huko kwa machafuko kunafungamyanishwa na kutia fora kwa askari zaidi 30.000 wa marekani walioanza kushika zamu hapo juni mwaka jana katika kile kilichoitwa „surge“.

Licha ya kutengenea kwa hali ya usalama kwa kadiri kubwa, makamanda wa kimarekani nchini Iraq wakionya watu kukaa macho na kwamba wafuasi wa madehehbu ya sunni wanaoungamkono Al qaeda ,bado ni hatari.

Jana tarakimu za serikali ya Iraq zilitaja kwamba raia 466 waliuwawa katika mashambulio mwezi uliomalizika wa Januari na idadi hiyo ni kasoro kuliko ile ya wairaqi 1,971 waliouwawa mwezi kama huo wa Januari,2007.

 • Tarehe 01.02.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D145
 • Tarehe 01.02.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D145