Miripuko ya bomu imeua watu 10 Uttar Pradesh
23 Novemba 2007Matangazo
Hadi watu 10 wameuawa katika mashambulizi ya bomu yaliyofanywa nje ya ofisi za mahakama katika miji mitatu ya Uttar Pradesh,kaskazini mwa India. Maafisa wamesema,miripuko hiyo imetokea katika miji ya Varanasi,Lucknow na Faizabad.Katika mripuko wa Varanasi wanasheria 7 walipoteza maisha yao na wengine 3 waliuawa katika mripuko uliotokea mjini Faizabad.
Maafisa wanawashuku wanamgambo wa itikadi kali za Kiislamu.Muda mfupi kabla ya mashambulizi hayo, ofisi ya wanasheria katika Jimbo la Uttar Pradesh iliamua kutowatetea tena washukiwa wa vitendo vya ugaidi.