1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mipango imekamilika ya kuiwekea Iran vikwazo vipya kuhusu Nuklia

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cy0H

VIENNA:

Wanachama watano wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa,mkiwemo Ujerumani, wakubaliana na hati ya pendekezo jipya ambalo litaitisha vikwazo zaidi kwa Iran kwa kukataa kusimamisha urutubishaji wa Uranium.Wanabalozi waliokaribu na shirika la nishati ya Atomic mjini Geneva wanasema Tehran imefichua mipango ya kuanza kufanya majaribio ya vifaa vipya vya kuhusiana na mpango wa matumizi katika nishati ya Nuklia.Licha ya Iran kukaidi baraza la usalama la umoja wa matifa-shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Nishati linaona alama ya Iran ya kutoa siri zake kama alama muhimu. Mkuu wa shirika la nishati la Umoja wa mataifa- Mohammed El baradei,ambae alitembelea Iran wiki mbili zilizopita, atatoa ripoti ya mazungumzo yake na viongozi wa Iran kwa shirika la nishati ya atomik la umoja wa Mataifa mwezi ujao.